Kufuatia sakata la jana la kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa wabunge saba wa upinzani, Mbunge wa Kigoma Mjini Mh Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa facebook kaweka msimamo wa chama chake(endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
CHAMA Cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu ndg. Zitto Kabwe.
Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa kwa sababu ya misimamo yao ya kutetea maslahi ya wananchi
Tungesikitishwa zaidi kama mashujaa wetu hawa wangeondolewa bungeni kwa sababu ya ulevi au wawe sehemu ya wagonga mihuri ya masuala ya hovyo hovyo yanayosimamiwa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)
Kwa sababu hiyo ya kusimamia maslahi ya wananchi sisi kwetu ni mashujaa na kwa maana hiyo Chama chetu kinaandaa maandamano makubwa jijini Dar Es Salaam kuwapokea mashujaa wa wananchi.
Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)