Ang'atwa uume na nyoka Thailand

Attaporn Boonmakchuay

Raia mmoja wa Thailand anaendelea kuuuguza jeraha katika hospitali moja baada ya nyoka aina ya<endelea bofya kichwa cha habari hii> chatu kutokea ndani ya choo na kumng'ata uume wake.

Attaporn Boonmakchuay,ambaye alipoteza damu nyingi amesema kuwa nyoka hiyo ilikuwa ikimvuta baada ya yeye na mkewe kujaribu kuipiga.

Madaktari wanasema kuwa Bw Attaporn ambaye alipoteza damu nyingi anaendelea vyema na matibabu.Nyoka akitolewa katika choo hicho

Wafanyikazi walilazimka kukiharibu choo hicho.Baadaye nyoka huyo aliachiliwa na kuingia msituni.

Kisa hucho kilitokea wakati ambapo Attaporn mwenye umri wa miaka 38 alielekea katika choo chake nyumbani kwake huko Chachoengsao,mashariki mwa Bangkok kabla ya kwenda kazini siku ya Jumatano.

Wakati alipokuwa akitumia choo hicho alihisi uchungu mkali.Nyoka aina ya chatu

''Nilihisi kama ambaye uume wangu ulikuwa umekatwa,Nyoka huyo alikuwa akinivuta kwa kutumia nguvu nyingi'',alisema.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top