Tundu Lissu : Tunakuja na staili mpya kumkabili Magufuli



Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa vyama vya upinzani vimejipanga vizuri kwaajili ya kukabiliana na Rais Dkt. John Magufuli .


Amesema hayo katika Semina iliyowashirikisha viongozi wa vyama vya upinzani kutoka Mataifa 16 iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni Jijini Dar es salaam, amesema wanapambana kuhakikisha uwanja wa siasa unakuwa sawa lazima wabadili staili ya kumkabili Rais Magufuli.


Lissu amesema watafanya siasa ikiwa Magufuli anataka ama hataki, ama wanavunja Sheria ama hawavunji” Akipiga marufuku shughuli za kisiasa, hatuwezi kwenda kanisani kuomba, hapana lazima kazi ziendelee katika aina nyingine”amesema Lissu.


Aidha, Lissu ameongeza kuwa katika Uchaguzi uliopita haukuwa wa haki na huru ambapo mawakala waliokuwa wakihesabu kura walikamatwa na kupelekwa polisi.


Hata hivyo ameongeza kuwa hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa kiongozi yeyote atakayefanya siasa anaonekana kama mhalifu na hukamatwa na kupelekwa mahakamani, hivyo hakuna Demokrasia bali kuna udikteta mkubwa.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top