Ziara Ya Makamu Wa Rais Mhe.samia Yawa Na Mafanikio Ukerewe


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye mji Nansio katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza mradi ambao utahudumia wananchi elfu 61.


Makamu wa Rais ambaye jana alisafiri kwa takribani masaa Matatu na meli ya MV Nyehunge II katika Ziwa Victoria kwenda kisiwa hicho kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo,aliwahimiza wananchi hao wautunze mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo na uhaba wa maji safi na salama katika kisiwa hicho.

Mradi huo ambao unaojumuisha kazi za uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unatekelezwa chini ya umefadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania katika miji ya Sengerema,Geita na Nansio – Ukerewe kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 30.4 ambapo serikali ya Tanzania imechangia mradi huo Dola za Kimarekani milioni nne.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliwaahidi wananchi kuwa serikali ya awamu ya Tano inamikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji.

Akihutubia mamia ya wananchi wa kisiwa cha ukerewe kwenye kijiji cha Kagunguli mkoani Mwanza mara baada ya kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ukiwemo mradi wa maji na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Kagunguli, Makamu wa Rais aliwapa pole wananchi wa kisiwa hicho baada ya kukumbwa na tufani ya kimbunga cha upepo iliyotokea tarehe 04 Novemba 2016 na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwemo nyumba za watu kubomoka.




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top