HAKIELIMU Yabariki Mabadiliko Katika Mafunzo Ya Ualimu Nchini


Kutokana na mabadiliko ya mafunzo ya ualimu yaliyo fanywa na Wizara ya Elimu ,Sayansi, Tektinolojia na ufundi novemba mwaka huu kuondoa mamlaka ya usimamizi wa ngazi ya cheti na stashahada kutoka Baraza la taifa elimu ya ufundi NACTE na kuyarudisha wizara ya Elimu chini ya uangalizi wa baraza la mitihani Tanzana NECTA, shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na Elimu nchini (HAKI ELIMU ) limeipongeza Serikali kwa hatua hiyo kwani hapo awali kwa kushirikiana na wadau wengine wa Elimu lilikuwa limesha toa mapendekezo kama hayo lakini hayakufanyiwa kazi.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, mkurugenzi mtendaji wa HAKI ELIMU ,Bwana John Kalage alisema mabadiliko hayo yatasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini,ingawa mabadiliko ya awali yalikuwa na lengo jema la kukabiliana na upungufu mkubwa wa waalimu wa kufundisha masomo ya Sayansi katika shule nyingi hapa nchini lakini yalikuwa na athari ya kuzorotesha ubora wa Elimu.


Alisema ,utaratibu wa kuvifanya vyuo vya elimu kujitegemea katika kudahili wanafunzi, kutathimini na kutunza waalimu tarajali ulikuwa pia na athali ya kushusha kiwango mafunzo ya ualimu kwakuwa kila taasisi iikuwa na uhuru wa kujiamulia viwango vya ubora wa mafunzo itakayo toa ,


“Katika zama hizi za ushindani kulikuwa na hatari dhahili kuwa kila taasisi ingeweza kudahili na kufaulisha wanafunzi wake hata wasio stahili ili kuvutia wana chuo wengi zaidi kwalengo la kujipatia ada ‘’alisema


Hatahivyo shirika hilo limetoa baadhi ya mapendekezo na kuishauri Serikali kuunda chombo chenye mamlaka ya juu katika elimu (Education Reguratory Authority ) chini ya sheria ya elimu ili kusimamia na kulinda sera ,sheria ,kanunu na miongozo ya elimu iliyo wekwa ili kupunguza maamuzi na mabadiliko ya mara kwa mara katika secta ya Elimu


“Kwa sasa ina onekana waziri ana mamlaka makubwa makubwa ya kutoa maamuzi hali inayo onekana kuwepo kwa nyaraka nyingi zinazo badilika kia mara hata kabla hazija fanyiwa kazi kikamilifu”


Kalage alisema nivema mafunzo ya ualimu ngazi zote yakaendelea kutolewa na vyuo vikuu na vyuo vya ualimu peke yake na vyuo vingine visivyo vya ualimu visiruhusiwe kutoa mafunzo hayo kwa kuwa lengo lao sikutoa mafunzo hayo .


"Nibora kuwa na vyuo vichachache ambavyo serikali ina uhakika na uandaaji wake ili vyuo hivi vilishe shule zote za umma na bnafsi ,hii itasaidia kuboresha kiwango cha elimu nchini."alisema 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top