Godbless Lema Akwama Tena Mahakamani Baada Ya Mawakili wa Serikali Kuweka Pingamizi, Amerudishwa Rumande Hadi Disemba 2


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo amefikishwa tena Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa ajili ya kusikiliza rufaa yake ya maombi ya dhamana.


Ulinzi ulikuwa umeimarishwa mahakamani hapo huku wafuasi wa Lema wakiwa wamevaa fulana nyeupe zilizoandikwa Jutice 4 Lema mbele zikiwa na picha yake.


Mbele ya Jaji Fatma Masengi aliyekuwa amepangwa kusikiliza Rufaa hiyo, Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J Marandu umeweka pingamizi kwamba mawakili wa Lema walipaswa kupeleka notisi ya rufaa kwanza na siyo kukata rufaa


Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wao wameshakamilisha taratibu zote za kisheria, hivyo wanasubiri uamuzi wa pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.


Jaji Fatma Masengi ameutaka upande wa serikali uwasilishe hoja za pingamizi lao kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.




Ulinzi ukiwa umeimarishwa

Advertisement

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top