Mechi ya kwanza bila kocha wao mkuu Hans van Pluijm, kikosi cha Yanga kimepata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu Stars ikiwa ni mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Kocha msaidizi Juma Mwambusi alisimama kwenye benchi la ufundi kutokana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo kujiuzulu kuifundisha timu hiyo.
Obrey Chirwa ameendeleza moto wake wa kufumania nyavu baada ya leo kupachika bao la kwanza dakika ya 6 lililoipa Yanga uongozi wa katika mechi hiyo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Mrundi Amis Tambwe alifunga bao la pili dakika ya 63 kabla ya Simon Msuva kuifungia Yanga goli la tatu dakika ya 83.
Tambwe alifunga goli la nne dakika ya 90+2 likiwa goli lake la pili kwenye mechi ya leo na kuhitimisha kipigo kingine siku chache baada ya kuishinda Kagera Sugar kwa goli 6-2 ugenini kwenye uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Dondoo
Yanga imeishinda JKT Ruvu kwa magoli manne katika mechi tatu za mwisho.
Yanga imefunga magoli 10 katika mechi mbili za mwisho. Kagera Sugar 6-2 Yanga na Yanga 4-0 JKT Ruvu Stars.
Wafungaji wa magoli ya leo jezi zao zina namba saba mgongoni. Obrey Chirwa (7), Simon Msuva (27) na Amis Tambwe (17).
Tambwe, Chirwa na Msuva tayari wameshafunga magoli 16 hadi sasa. Tambwe (6), Chirwa (5) na Msuva (5).
Obrey Chirwa amefunga magoli matano katika mechi nne alizocheza. Amefunga mfululizo kwenye mechi tatu za mwisho. Alianza kufunga kwenye mchezo wa Yanga 3-1 Mtibwa, mchezo wa Azam vs Yanga hakufunga ulimalizika 0-0, akafunga kwenye mechi ya Toto Africans 0-2 Yanga, Kagera Sugar 2-6 Yanga na leo October 26 Yanga 4-0 JKT Ruvu Stars.
JKT Ruvu imepoteza mfululizo mechi zake tatu za mwisho, ilifungwa na Ruvu Stars 0-1 Kagera Sugar, Azam FC 1-0 JKT Ruvu na Yanga 4-0 JKT Ruvu.
JKT Ruvu ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 9 baada ya kucheza mechi 15 ikiwa imeshinda mechi moja pekee.
Yanga ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 11 imefikisha pointi 24 pointi tano nyuma ya vinara wa ligi Simba SC.
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 29 & 30 bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)