Kilimanjaro Queens walipata mabao yao kupitia kwa Amina Ally pamoja na Asha Rashid aliyefunga mabao mawili.
Rwanda kwa upande wao, walipata mabao yao kupitia kwa Ibangarrye Anne Marrie pamoja na Stumai Abdallah ambaye alijifunga.
Michuano hiyo inashirikisha timu nane ambazo ni wenyeji Uganda, Kenya, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Zanzibar, Sudani Kusini na Tanzania Bara.
Timu hiyo iko chini ya kocha mkuu Sebastian Nkoma katika mashindano hayo ya kwanza kufanyika ukanda huu yakihusisha timu za wanawake.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)