Mmiliki Mwenza Wa Jamii Forum Apandishwa Kizimbani


Mmiliki mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kuunganishwa katika mashtaka yaleyale yanayomkabili mkurugenzi wa kampuni hiyo, Maxence Melo.


Washtakiwa wote wawili walisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na Hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa.


Wakili wa serikali, Mohamed Salum alisema kuwa washtakiwa hao wakiwa eneo la mikocheni kwa nafasi zao wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa mawasiliano kwa njia ya mtandao kufuatia chapisho lililochapishwa katika tovuti yao waliamua kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi kwa kuwanyima data walizonazo.


Hata hivyo upelelezi wa kesi hizo mbili umekamilika na washtakiwa wote hawa watasomewa mashataka yao kuanzia Februari 9 na Februari 20.

Mpaka sasa washtakiwa wote wawili wapo nje kwa dhamana kwa masharti ya bondi ya Milioni 10 kwa kila kosa na masharti ya kutosafiri nje ya nchi.

Maxence Melo akimweleza jambo mmiliki mwenza wa Jamii Forum Mike mushi ndani ya chumba cha Mahakama

Maxence Melo na Mike Mushi wakimsikiliza wakili wao

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top