Baada ya kuanza mazoezi mkoani Morogoro, kocha msaidizi wa Simba SC Jackson Mayanja amesema, wanatarajia kufanya mazuri kama walivyofanya katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara.
“Wachezaji wote wameenea tumeanza mazoezi yetu, tunaendelea na mazoezi yetu tuliyoanza nayo Dar kila mtu ypo vizuri na kambi ipo safi.”
“Timu yenye wachezaji 25, wakifika wachezaji 23 au 24 timu inakuwa kama imeenea. Kama mchezaji mmoja anashida za kifamilia akimaliza matatizo yake ataungana na timu.”
“Wanasimba wanachotaka ni kuona tunacheza na kushinda kama hatushindi basi inakuwa bahati mbaya lakini kikubwa ni kupata pointi katika kila mechi.”
“Tutaendelea kuongoza kama tutakuwa tunaendelea kushinda mechi hakuna kingine.”
Kikosi cha Simba kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya Polisi Morogoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara kabla ya kuanza kwa raundi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara. Mchezo huo utachezwa December 9 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)