NA
Na John SM Mgejwa (The economist)
Kumekuwa na maandamano nchini Marekani tangu uchaguzi umalizike juzi 8 na 9 November, ambapo miamba miwili ilichuana sana toka kwenye kampeni hadi kwenye upigaji kura. Juzi juzi tu tulishuhudia Trump akitangazwa mshindi kwa kura 276 za wajumbe na kumshinda Mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Hillary Clinton.
Kumezuka maandamano makubwa nchini Marekani kupinga kuchaguliwa Trump, maandamano haya hayamaanishi kuwa hakuchaguliwa kihalali au kura ziliibwa kama ilivyozoeleka barani Afrika, bali baadhi ya wamarekani hawamtaki kutokana tu na matamshi yake ya kuudhi na kuashiria mvurugano pindi atakapoapishwa January 20, 2017.
Sitaki kuongelea sana ushindi wake kwani Mimi sikuwa na upande wowote kwa hao wawili wagombea urais, na hii ni kwa sababu zangu binafsi kulingana na hali ya dunia ilivyo kwa sasa maana niliamini na hadi leo naamini, vyama vyote viwili havikuweza kuleta wagombea sasa kulingana na record ya dunia ilivyo sasa.
Katika maandamano tumeshuhudia wamarekani wakibeba mabango yaliyoandika "call an California exit from the USA.
Watu kutoka California wameanza kuonyesha viashiria vya kujitenga kutoka katika muungano wa America kama walivyofanya WAINGEREZA na baadaye Waskochi,
KWA NINI CALIFONIA INATISHIA HIVYO??
HEBU TUONE CALIFORNIA NI KITU GANI PALE MAREKANI NA DUNIA!!!
California ni jimbo la tatu kwa ukubwa wa eneo nchini Marekani kati ya majimbo 50 ya nchi hiyo, California linaukubwa wa 423, 970km za mraba sawa na 163,696 square miles.
California lina upana wa km 400 na urefu wa 1240km. Jimbo hili 4.7% ni maji. Pato la wastani kwa mtu mmoja mmoja ni $67,458 na kwa GDP PER CAPITA HII ni jimbo la tatu nchini Marekani.
California ina watu 39, 144, 816, idadi ambayo inalifanya jimbo hili kuwa la kwanza kwa idadi kubwa ya watu nchini Marekani kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2005.
California iliwahi kukaliwa na makabila (wazawa) mbalimbali ya kiamerika kabla ya kugunduliwa na watafiti wa ulaya katika karne ya 16 na 17. Spain empire iliwahi kudai kuwa California ni sehemu ya Alta California ambayo ilikuwa chini ya himaya ya Hispania (new). Na pamoja na hayo ni kwamba hii Alta California ilikuwa sehemu ya Mexico mnamo mwaka 1821, baada ya vita ya Uhuru Mexico iliirudisha hiyo sehemu na kuiondoa mikononi mwa New Spain.
Mwaka 1848 ilitokea vita Kali kati ya Mexico na Marekani hii vita ilijulikana sana kwa jila la Mexican-American war, enzi hizo marekani ilikuwa tayari ni muungano wa majimbo 30, vita hii ililihusu eneo la California lililokuwa sehemu ya Mexico, Marekani ilipigana kwa nguvu zote na kuliweka chini ya himaya yake, hali ambayo ilileta shida kati ya Marekani na Mexico, na nafikiri haya mambo hayajawahi kuisha.
Baada ya marekani naweza kusema kupora eneo hilo la California, iliamua kuisainisha au kuisajili kama jimbo la US tarehe 9 September, 1850. Hivyo California likawa jimbo la 31 katika muungano wa America.
Katika suala la kisiasa, California inaongozwa zaidi na chama cha akina Obama, Democratic party, mfano California, governor wake Jerry Brown anatoka chama cha akina Obama, lieutenant Governor bwana Gavin Newsom anatoka chama cha Democratic cha akina Obama, na bado katika bunge la Marekani, maseneta wanao iwakilisha California wote Dianne Feinstein na Barbara Boxer wanatoka Democratic party cha akina Obama, hapa sasa utaona ni namna gani Democratic ni chama kinachoiongoza California.
California inachangia katika uchumi wa marekani kwa zaidi ya 58% , a populous county "Los Angeles inaptikana jimboni California, hii ni sehemu ya kuvutia ukienda marekani usipofika Los Angeles basi utajilaumu sana, San Bernardino county nayo inapatikana kule,
California ndiko yaliko maskani ya makampuni 3 makubwa yenye mapato makubwa kati ya 20 Duniani, makampuni hayo ni CHEVRON, APPLE, NA McKesson, California ndiko ambako filamu industry, internet na computer binafsi vilianzia. Uchumi wake unategemea sana utalii, ukusanyaji wa kodi, kilimo katika central valley, biashara ya kitaalamu, real estate services teknolojia na utaalamu usio kifani.
California imebahatika kuwa na mabonde mazuri kwa kilimo kama vile central valley, ambapo kilimo chake pamoja na kwamba kinachangia kwa 1.5% katika uchumi wake bado kwa USA inachangia sana kuliko jimbo lolote lile.
California na mexico wana share international border hivyo hii nayo inaweza kuleta mgogoro kuhusu ukuta unaoongelewa na bwana Trump.
Jimbo hili pamoja na ufahari wake liko katika Pacific ring of fire hali ambayo insababisha kwa mwaka matetemeko madogo madogo ya ardhi kurekodiwa na kufikia 37,000 ingawa huwa Mara nyingi huwa hapana madhara.
Wacalifonia wanapotaka kujiondoa wanajua dhahiri kuwa jimbo lao ndiyo linaonekana kwa kiasi kikubwa kuchangia katika uchumi wa marekani,
Wachambuzi wa mambo wanasema kama California ingekuwa nchi inayojitegemea, uchumi wake unashikiria nafasi ya 6 duniani na kwa umaarufu ni nchi ya 35 duniani, umaarufu ambao unatokana na mji wenyewe kuwa na vivutio vingi.
Wacalifonia "California republic" wameanza chokochoko hizi, za kutaka kujiengua Marekani kwa sababu wanaamini jimbo lao linaweza kujitegemea kama nchi, kwa sababu mpaka sasa ikichukuliwa kama nchi basi inashikiria namba 6 kwa uchumi duniani, hata Tanzania haikaribii hata kwa 0.000005
Tuwaombeee tu wasiendelee na Mawazo hayo maana inaweza kuleta hata mtafaruku mkubwa na pia mexico yawezekana wakawakumbusha watu wa California kuwa nyinyi ni wa kwetu hivyo rudini tuungane ili kumdhoofisha Donald Trump na wazo lake la ukuta.
By John SM Mgejwa (The economist)
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)