Trump kuwatimua wahamiaji haramu milioni 3 kutoka Marekani

Wasiyemtaka ameingia ikulu ya Marekani na kama walikuwa wakidhani vitisho alivyokuwa akivitoa wakati wa kampeni vilikuwa ni mkwara tu, wanapaswa kujipanga upya!


Ni kwasababu Rais Mteule wa nchi hiyo, Donald Trump ameusisitizia msimamo wake dhidi ya wahamiaji haramu nchini humo. Amedai kuwa ana mpango wa kuwafungashia virago wahamiaji haramu takriban milioni tatu,hasa wale wenye rekodi ya uhalifu.


Amesisitiza pia kuwa mpango wa kujenga ukuta upo pale pale.


Katika mahojiano yake ya kwanza tangu ashinde uchaguzi na kuja kuchukua kijiti cha Urais toka kwa Barack Obama, Trump amewahakikishia wafuasi wake kuwa atawatimua wahuni na wauzaji wa madawa ya kulevya wote toka Marekani.


Katika mahojiano kwenye kipindi cha CBS, 60 Minutes, Jumapili jioni, Trump amesema atajenga ukuta kutenganisha Mexico na Marekani kama alivyoahidi kwenye kampeni yake.


Kuna wahamiaji haramu takriban milioni 10 nchini Marekani.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top