Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27 Oktoba, 2016 amemteua Bw. Samwel Peter Kamanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Bw. Samwel Peter Kamanga ameteuliwa kushika wadhifa huo kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2016.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Samwel Peter Kamanga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)