Utata wa kisheria umemkwamisha Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya kutoa ushahidi katika kesi ya kutetea ubunge wake inayoendelea mjini Musoma.
Hatua hiyo ilitokana na malumbano ya kisheria kati ya mawakili wa upande wa waleta maombi na wa utetezi hali iliyosababisha Jaji Noel Chocha anayesikiliza kesi hiyo kuiahirisha hadi leo mchana.
Utata huo uliibuka baada ya wakili Constantine Mutalemwa wa upande wa waleta maombi kuweka pingamizi katika baadhi ya aya kwenye hati ya kiapo cha shahidi huyo hatua iliyozua mjadala mkubwa kati yake na wakili wa upande wa utetezi Tundu Lissu.
Katika mjadala huo mahakani jana, kila wakili alijaribu kutetea hoja yake na kutoa vifungu vya sheria ambavyo vinaonyesha msingi wa hoja walizokuwa wakitoa.
Wakili Mutalemwa amesema aya hizo ambazo aliiomba mahakama ziondolewe zilikuwa zinapingana na matakwa ya kanuni na sheria za kuongoza mashauri ya kesi za madai ya uchaguzi.
Mutalemwa alisema kati ya aya 11 zilizosomwa na mjibu maombi wa kwanza katika kiapo chake zinazotakiwa kubaki katika kiapo hicho ni aya nne ambazo alisema hazina utata wowote.
Alizitaja aya ambazo zilitakiwa kuondolewa kwenye kiapo hicho cha shahidi wa kwanza kuwa ni pamoja na aya ya 2,3,4,5,6,7,8 ambazo zilikuwa zinaibua hoja mpya ambazo hazikutajwa kwenye majibu yao wakati wakijibu maombi katika hatua za awali. Hata hivyo, hakufafanua kilichomo kwenye aya hizo.
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano October 12, 2016 bofya hapa
PICHA 5: Tingatinga Lilivyofukua mamilioni yaliyokuwa Yamefichwa ardhini bofya hapa
Waziri atolea maelezo taarifa ya serikali kuhakiki watumishi wanavyotumia mishahara yao bofya hapa
Waziri atolea maelezo taarifa ya serikali kuhakiki watumishi wanavyotumia mishahara yao bofya hapa
TCRA yakipa onyo kali kituo cha runinga cha Clouds, Yakifungia kwa miezi 3 kipindi cha 'Take One' kwa kukiuka kanuni za utangazaji. bofya hapa
Polisi Aliyerekodiwa Akipokea Rushwa Kuchukuliwa Hatua bofya hapa
Jeshi La Polisi Nchini Latoa Onyo Kali Kwa Wananchi Wanaojichukulia Sheria Mkononi. bofya hapa
Polisi Aliyerekodiwa Akipokea Rushwa Kuchukuliwa Hatua bofya hapa
Jeshi La Polisi Nchini Latoa Onyo Kali Kwa Wananchi Wanaojichukulia Sheria Mkononi. bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)