PLUIJM AITANGAZIA KIAMA KAGERA SUGAR,ATAJA MIKAKATI YAKE ,CHIRWA KUONGOZA MASHAMBULIZI LEO



Na.Alex Mathias.

Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto African ya jijini Mwanza,Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Hans Van Der Pluijm ameitangazia vita Kagera Sugar zitakapokutana Leo kwenye uwanja wa Kaitaba mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Akizungumza baada ya kutua mkoani Kagera Pluijm,amesema kuwa anategemea mchezo utakuwa mgumu kwa kila timu kutafuta alama tatu muhimu na ukiangalia wenyeji nao wana alama 18 sawa na sisi ila hilo halitupi shida.

“Kila mechi kwetu tunaichukilia kwa uzito wa aina yake na ukiangalia kikosi changu bado kina uchovu wa mashindano ya kimataifa ndio maana najaribu kufanya mabadiliko mbalimbali ili kuwapa nafasi wachezaji wote wacheze”alisema Pluijm

Timu hizo zinatarjia kukutana Leo huku zikiwa zote zimetoka kupata ushindi Kagera waliwafunga Maafande wa JKT Ruvu kwenye uwanja wa Mabatini wakati Mabingwa watetezi wao waliwafunga wadogo zao Toto mabao 2-0.

Hata hivyo Kocha huyu hakuacha kumsifia mshambuliaji wake raia wa Zambia Obrey Chirwa kwa kuanza kuzoea Ligi na kuanza kujiamini na kufunga magoli mpaka sasa anayo mawili na kuondoa presha za mashabiki ambao walikuwa wanaomuona kama sio mchezaji mzuri. Kagera Sugar wanawakaribisha mabingwa wao wakiwa chini ya Kocha mpya Mecky Mexime na wakiwa nafasi ya nne kwa alama 18 wakati Yanga wapo nafasi ya tatu kwa alama 18 huku kinara bado Simba anaongoza kwa alama 24
 
 
 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top