AUDIO: Yanga yatii agizo la mahakama, yasitisha mkutano mkuu




Siku moja baada ya mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kuwatangazia wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa dharura uliopangwa kufanyika Jumapili October 23,
leo amesitisha mkutano huo baada ya kupokea agizo kutoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Manji amesema, kufanya mkutano huo wakati wamepokea agizo halali la mahakama kusitisha mkutano huo, itakuwa ni kinyume cha sheria za nchi.

“Nimepokea hukumu ya mahakama ya Kisutu ikisema mkutano wa Yanga usifanyike Jumapili (kesho) ilibidi tuhakikishe kama ni kweli na siyo hukumu bandia,” amesema Manji wakati akitoa tamko la klabu kuhusu agizo la mahakama kufuta mkutano mkuu wa dharura.

“Baada ya kuthibitisha ile hukumu ni kweli, natoa taarifa kwa wanachama wa Yanga kwamba mkutano hautakuwepo. Mkutano wa kesho mahakama ya Kisutu imetuzuia kufanya, imetusikitisha kwasababu kuna watu wengine wako njiani wanakuja kutoka Mbeya, Mwanza, Zanzibar na sehemu nyingine nyingi nawaomba radhi na nawapa pole.”

“Tukifanya mkutano tutakuwa tunavunja sheria, hii klabu ambayo mimi nimepewa dhamana ya kuiongoza kama Mwenyekiti wake lazima ifate sheria za nchi yetu. Vitu vingine hatutaweza kukubaliana navyo tutapinga lakini sisi ni watu ambao tunafata sheria hatuwezi kuwa watu ambao hatuheshimu sheria za nchi yetu.”

“Naomba wana Yanga kesho wasije wakadhani kutakuwa na mkutano, dola inaweza kuwachukulia kama wanavunja sheria. Katiba yetu tunaijua mtu akienda mahakamani kwenye mambo ya klabu si mwanachama. Tunaimani mahakama itafanya kitu sahihi.”

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top