AUDIO: Mrithi wa Van Pluijm ameikana Yanga aeleza kilichomleta




Kocha mzambia George Lwandamina anayetajwa kujiunga na klabu ya Yanga kuchukua nafasi ya Hans van Pluijm amekanusha taarifa hiyo kwa kusema hajafanya mazungumzo na klabu yeyote
ya Tanzania huku akisisitiza kuwa, ujio wake nchini ni kwa ajili ya shughuli zake binafsi za kibiashara.

Lwandamina amesema Tanzania sio ya Yanga pekeyake, mtu yeyote anaweza akaja kwa shughuli zake binafsi lakini yeye amekuja kibiashara. Zambia na Tanzania sio mbali na kuna raia wengi wa Zambia hapa nchini lakini hajapata ofa kutoka klabu yeyote ya Tanzania ingawa alipata ofa ya kufundisha Afrika Kusini pamoja na Congo DR.

“Kuna mambo mengi yanaendelea Tanzania kwahiyo ujio wangu si kwa ajili ya Yanga pekee, nimekuja kufanya mambo yangu ya kibiashara kama unavyojua Zambia ni nchi ambayo haina bandari kwahiyo kuna mambo mengi yanaendelea hapa na ukitaka kufanya bishara, Tanzania ndio bandari iliyo karibu zaidi na Zambia.”

“Ninauhakika kuwa hapa kuna raia wengi wa Zambia, kwa hiyo na mimi naungana nao. Kwa upande mwingine mimi ni kocha mwenye weledi, ninaweza kufundisha soka popote sio Tanzania pekee hata nyumbani kwetu Zambia endapo kuna ofa inatokea tunakaa mezani na kuzungumza.”

“Hakuna klabu yeyote ya Tanzania niliyofanyanayo mazungumzo, nilipata ofa kutoka Afrika Kusini siwezi hata kutaja ni timu gani, nilipata ofa pia nchini Congo DR lakini siyo Tanzania.”

Huenda Lwandamina hataki kuthibitisha kujiunga na Yanga hadi hapo uongozi wa klabu hiyo utakapotoa taarifa rasmi ya kuinasa saini yake na kumtangaza rasmi kuwa kocha wao mpya. Tayari uongozi wa Yanga umethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa kocha wao Hans van Pluijm, huenda Lwandamina akatangazwa muda wowote kwa ajili ya kuiongoza timu kwenye mechi zake za ligi kuu Tanzania bara inayozidi kusonga mbele.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright 2025 UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top