
Nilimuuliza Himid kuhusu nafasi ya Azam kwenye mbio za ubingwa ligi msimu huu wakiwa wamecheza mechi tano na kufanikiwa kuvuna pointi 10 baada ya kushinda michezo mitatu sare moja na kupoteza mchezo mmoja.
“Ni mapema sana kuzungumzia masuala ya ubingwa, cha muhimu ni kupambana kila game round ya pili tutaanza kuzungumzia habari hizo”, amesema nahodha msaidizi wa Azam Himid Mao ambaye alichezeshwa nafasi ya beki ya kati dhidi ya Simba.
“Tulicheza vizuri sana nawapongeza wachezaji wenzangu, kupoteza mechi ni sehemu ya mchezo hakuna kibaya chochote tulichofanya. Malengo ya timu yeyote ni kushinda kila mchezo lengo letu katika mchezo wowote ni kushinda japo unapoingia kwenye mechi chochote kinaweza kutokea.”
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)