UKIMUULIZA HIMID KUHUSU UBINGWA WA VPL, HILI NDIYO JIBU LAKE

Kiungo wa Azam FC Himid Mao Mkami amesema ni mapema sana kuzungumzia habari za ubingwa wa VPL msimu wa 2016-17 kwasababu ligi bado iko mwanzoni, nyota huyo wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ anasema kila wanapoingia uwanjani leongo lao ni kushinda lakini kushindwa kuchomoka na pointi tatu ni moja ya matokeo ya soka.

Nilimuuliza Himid kuhusu nafasi ya Azam kwenye mbio za ubingwa ligi msimu huu wakiwa wamecheza mechi tano na kufanikiwa kuvuna pointi 10 baada ya kushinda michezo mitatu sare moja na kupoteza mchezo mmoja.

“Ni mapema sana kuzungumzia masuala ya ubingwa, cha muhimu ni kupambana kila game round ya pili tutaanza kuzungumzia habari hizo”, amesema nahodha msaidizi wa Azam Himid Mao ambaye alichezeshwa nafasi ya beki ya kati dhidi ya Simba.

“Tulicheza vizuri sana nawapongeza wachezaji wenzangu, kupoteza mechi ni sehemu ya mchezo hakuna kibaya chochote tulichofanya. Malengo ya timu yeyote ni kushinda kila mchezo lengo letu katika mchezo wowote ni kushinda japo unapoingia kwenye mechi chochote kinaweza kutokea.”
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top