
Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu mara moja kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Ameambia Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana na changaomoto za kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.
''Ni wazi kwamba umri wake na hali ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza kulinusuru taifa hilo''.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.
Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.
Khama anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu.
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo alhamis september 22, 2016 bofya hapa
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo alhamisi september 22, 2016 bofya hapa
PICHA 12 NDANI NA NJE ZA NDEGE MPYA BOFYA HAPA
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo alhamisi september 22, 2016 bofya hapa
PICHA 12 NDANI NA NJE ZA NDEGE MPYA BOFYA HAPA
Ndege mpya ya ATCL yatua nchini, utaratibu wa mapokezi rasmi wapangwa bofya hapa
Nafasi za kazi bofya hapa
Nafasi za kazi bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)