Mtemvu abwagwa kesi ya uchaguzi Temeke



Aliyekuwa Mbunge wa Temeke (CCM) Abbas Mtemvu, ameshindwa kesi ya uchaguzi dhidi ya Abdallah Mtolea(CUF) aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.


Mtemvu aliyekuwa akitetea kiti hicho katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alifungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akipinga matokeo yaliyompa ushindi Mtolea.


Pamoja na mambo mengine akidai kuwa kura za baadhi ya vituo vya kupigia kura hazikujumlishwa katika matokeo ya jumla.


Hata hivyo Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa leo na Jaji Issa Maige aliyekuwa akisiliza kesi hiyo imetupilia mbali madai ya Mtemvu na badala yake imemthibitisha Mtolea kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.


Katika hukumu hiyo Jaji Maige amesema kuwa Mtemvu ameshindwa kuthibitisha madai yake jinsi yalivyoathiri ushindi wa mbunge huyo, huku akisema kwamba kasoro alizokuwa akizilalamikia Mtemvu hakuathiri ushindi wa mbunge huyo.


abari zilizopo katika Magazeti ya leo alhamis september 22, 2016 bofya hapa 
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo alhamisi september 22, 2016 bofya hapa

PICHA 12 NDANI NA NJE ZA NDEGE MPYA BOFYA HAPA





 



Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top