
Moja ya malori yaliyoteketezwa
Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano.
Wamarekani wamekuwa wakiamini kuwa Urusi ndio iliyoshambulia msafara huo, huku Warusi wakilipinga hilo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi John Kerry, alitoka nje ya lugha ya kidiplomasia kwa kutumia dhihaka zaidi. Huku mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov akipinga hisia hizo kali kwa kuorodhesha mifano kadhaa kutetea nchi yake. Aidha ametaka pia kufanyika
Licha ya majibizano makali, Urusi na Marekani zilikubaliana kwa pamoja kuongoza mkutano wa mataifa 23, yanayoiunga mkono Syria ambao utafanyika mjini New York, baadaye leo.
Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umesema unajiandaa kuanza tena kutoa misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria, baada ya kusitishwa kwa usambazaji wa misaada kufuatia shambulio hilo.
Mjumbe wa Umoja wa Mnataifa nchini Syria, Staffan de Mistura ameiambia BBC kwamba misafara hiyo ya misaada itaanza katika baadhi ya maeneo lakini kwa uangalifu na tahadhari kubwa. Misaada hiyo amesema haitasambazwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Aleppo, ambalo limeshambuliwa vibaya.
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo alhamis september 22, 2016 bofya hapa
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo alhamisi september 22, 2016 bofya hapa
PICHA 12 NDANI NA NJE ZA NDEGE MPYA BOFYA HAPA
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo alhamisi september 22, 2016 bofya hapa
PICHA 12 NDANI NA NJE ZA NDEGE MPYA BOFYA HAPA
Ndege mpya ya ATCL yatua nchini, utaratibu wa mapokezi rasmi wapangwa bofya hapa
Nafasi za kazi bofya hapa
Nafasi za kazi bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)