Mfanyabiashara Christon Mbalamula, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kudai anatangaza ndoa na askari watakaomhudumia kama mume, huku akihoji kama wameshanunua mafuta ya kilainishi maarufu KY.
Mshtakiwa huyo alifikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana akikabiliwa na shtaka la kutumia huduma ya mtandao wa kijamii wa ‘WhatsApp’ kulidhalilisha jeshi hilo.
Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Dk. Yohana Yongolo, Wakili wa Serikali, Winifrida Sumawe alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 26 mwaka huu katika eneo la Vijibweni Kigamboni.
Alidai siku ya tukio, mshtakiwa alilidhalilisha Jeshi la Polisi baada ya kutumia huduma ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp kusambaza ujumbe unaosema. “Natangaza ndoa na askari yoyote atakayejipendekeza kwangu siku hiyo ataolewa bila mahari.
“Ataishi kwangu bila nguo hadi operation Ukuta itakapoisha atapika na kupakua na kunikidhi haja km mume wake, Note KY JELLY mmeishanunua so msiogope nyie mapolice uchwara” alisema katika ujumbe huo.
Mshtakiwa huyo alikana shitaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.
Hakimu Yongolo alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, kila mmoja asaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni moja na mmoja kati ya wadhamini hao awe na mali isiyohamishika yenye thamani isiyo chini ya Sh milioni mbili. Mshtakiwa awe anaripoti kila baada ya wiki mbili kwa msimamizi wa mawakili wa serikali.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)