Baada ya kuzushiwa kifo, Bilionea Dangote ameyaandika haya.


Bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote amekanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia akiwa nchini Ujerumani.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa bilionea huyo amefariki akiwa nchini Ujerumani baada ya kuugua kwa muda mfupi. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa familia ya bilionea huyo imethibitisha kifo cha ndugu yao huyo na kusema kuwa ni pigo kubwa kwa Afrika.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dangote ameandika hivi “I am hale, hearty and alive. Please disregard malicious report saying otherwise. Thank you.” , akimaanisha kuwa yeye ni mzima wa afya na kuwataka watu kupuuzia taarifa zinazoeleza kivingine.”


Akimaanisha “Mimi ni mzima na buheri wa afya. Tafadhali puuzeni taarifa zote zinazosema vinginevyo. Asanteni.”


Aliko Dangote ni raia wa Nigeria, ndiye mwenye utajiri mkubwa zaidi barani Afrika. Dangote anamiliki kampuni kubwa ya Dangote Group inayofanya kazi katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwa ni pamoja na Nigeria, Benin, Ethiopia, Senegal, Cameroon, Ghana, Afrika Kusini, Togo, Tanzania na Zambia.


Muda mfupi baada ya kuzuka kwa taarifa hizo, Aliko Dangote alikanusha taarifa hizo kupitia mtandao wa Twitter kwa kupost kuwa yuko Afrika kusini na yuko salama kabisa.
 
 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top