Mgoli ya Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo yameipa Simba pointi tatu dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Ruvu Shooting ambao ndio wamepoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Simba katika mechi tatu walizocheza, walianza kupata goli lililofungwa na Abulrahman Mussa dakika ya saba kipindi cha kwanza.
Ajibu aliisawazishia Simba goli hilo dakika nne baadaye na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana bao 1-1.
Mavugo aliifungia Simba bao la pili na la ushindi dakika ya 48 kipindi cha pili akimalizia pasi ya Ibrahim Ajib.
Matokeo ya mkoani Mbeya
Azam ikiwa mkoani Mbeya imeifunga Tanzania Prisons goli 1-0 kwenye uwanja wa Sokoine.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)