Mara baada ya wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania bara kukabidhi vifaa kwa timu shiriki kuelekea katika msimu ujao wa ligi unaotaraji kuanza kutimua vumbi agost 20 mwaka huu,hii leo uongozi wa Yanga umeibuka na kusema kwamba kwa upande wao hawatazitumia jezi hizo kwa kua hazina ubora unaolingana na hadhi ya klabu
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,mkuu wa kitengo cha masoko na mratibu wa matawi,Omar Kaya amesema kwamba jezi ambazo zimeonyeshwa jana na wadhamini wa ligi kuu hazina ubora unaolingana na timu na anashangaa kuona wanatoa jezi ambazo zilitumika katika msimu uliopita
Amesema kwamba hata mchakato wa upatikanaji wa jezi hizo za nyumbani na ugenini hakuna kiongozi yeyote wa Yanga aliyehusishwa hivyo uongozi unashangazwa na hatua hiyo kwani mpango wao kwa sasa ni kubadilisha mfumo wa jezi ili waanze mchakato wa biashara ya jezi.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)