WANAFUNZI WANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO SHULE YA SEKONDARI SADANI MUFIND


Mkuu wa wilaya ya mufindi akikabidhi kwa mwanafunzi godoro alipo wasili na viongozi wa halmashauri shuleni saadani usiku wa
agosti 01



Mkuu wa Wilaya, mbunge na mwenyekiti wa Halmashauri wakiangalia bweni lililo ungua.

Jumla ya wanafunzi 50 wa shule ya Sekondari Sadani iliyopo halmashauri ya wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wamenusurika kuteketea kwa moto baada ya moja kati ya mabweni ya wasichana wa shule hiyo kushika moto na kuteketeza mali zote zilizokuwa ndani ya bweni hilo.

Taarifa ya iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imeeleza kuwa moto ambao chanzo chake hakijafahamika mara moja uliibuka ghafla julai 31 majira ya saa moja na nusu usiku na kuteketeza vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 09 na laki 06

Taarifa hiyo imebainisha baadhi ya vitu hivyo kuwa ni pamoja na vitanda, magodoro, blanketi na mabati na kuongeza kuwa hakuna mwanafunzi yeyote aliyepoteza maisha na tayari vyombo vya usalama vimeanza uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Aidha, uongozi wa halmashauri ya Wilaya ukiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamuhuri William, Mwenyekiti wa Halmashauri Festo Mgina na Mbunge wa jimbo la Mufindi kasikazini Mahamudu Mgimwa, ulifika shuleni hapo mapema agasti moja kutoa pole na kukabidhi mahitaji muhimu ya wanafunzi yenye thamani ya Shilingi milioni 06 kisha wakazungumza na wanafunzi. Hii ni ajali nyingine ya moto katika mabweni ya wasichana Mkoani Iringa kwani manamo mwaka 2009 ajali mbaya zaidi ilitokea katika shule ya sekondari Idodi Wilayani Iringa na kusababisha vifo vya wanafunzi 12

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top