UVCCM waanza kutumbuana, baadhi wasimamishwa wengine wafukuzwa kazi.


UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani hapa, umewasimamisha kazi na kuwafukuza viongozi wake wa Mkoa wa Iringa huku aliyekuwa Katibu Mkuu wa umoja huo, Sixtus Mapunda, akipelekwa mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ili aweze kujadiliwa.

Mapunda ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Mjini (CCM), anatuhumiwa kukwapua hati za viwanja vya UVCCM bila idhini za vikao husika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema viongozi hao wamesimamishwa na wengine kufukuzwa kazi kutokana na tuhuma za kuuza shamba linalomilikiwa na umoja huo lililopo eneo la Igumbilo mkoani Iringa.

Alisema ripoti ya uchunguzi inaonesha kuwa shamba la UVCCM namba 454 lenye ekari 2,10 l limeuzwa kwa mtu aliyetambulika kwa jina la Suhail Ismail kinyume cha sheria na utaratibu wa chama.

Alisema Baraza Kuu la UVCCM Taifa linamsimamisha Seki Kasuga, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM na Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Mkoa wa Iringa.

Mbali na vigogo hao mwingine aliyekumbana na tumbuatumbua hiyo ni Mkuu wa Idara ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha, Omar Suleiman ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mjini- Zanzibar.

“Pia yupo Ally Nyawenga ambaye alikuwa Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Mkoa wa Iringa. Huyu amefukuzwa kazi kwa kuuza viwanja vya UVCCM kisha kuzigawa fedha alizozikusanya kwa baadhi ya viongozi wa CCM.

“Baraza Kuu la UVCCM Taifa limeiagiza sekretarieti ya UVCCM kumwandikia barua ya kumfukuza kazi Upendo Kinyunyu ambaye ni Katibu Muhtasi ambaye kwa makusudi aliamua kupotosha taarifa zote alizotoa kwa kamati ya uchunguzi ili kamati ishindwe kubaini ukweli,” alisema Shaka.

 
 
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu August 15, 2016 bofya hapa


 Ajira zaidi bofya hapa


Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA



Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top