Trump ajikita kuboresha uchumi wa Marekani



Donald Trump
  Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump amebadilisha mwelekeo wa kampeni zake na kujikita kwenye masuala ya uchumi baada ya wiki ngumu ya kuanza kampeni za uchaguzi
.Trump akiwa mjini Detroit ameahidi kuibua uchumi wa Marekani kwa mwendo wa kasi kwa kufuta kodi za mashirika endapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo mwezi Novemba. 

Amesema nafasi nyingi za kazi zitatengenezwa kwa mabadiliko hayo ya mfumo wa kodi sanjari na makubaliano mapya ya mkataba wa kibiashara wa kanda ya Marekani ya Kaskazini.

Mabadiliko niliyoyaelezea leo ni ya mwanzo tu. Tutakapofanya mabadiliko katika mfumo wetu wa kodi, biashara, nishati na sera za uthibiti, tutakuwa tumefungua ukurasa mpya kabisa, tutakuwa tumefungua ukurasa mpya katika maendeleo ya Marekani, ambayo yanahitajika sana. Tunahitaji ukurasa mpya. Donald Trump, Mgombea Urais wa Marekani-Republican

Trump amesema kupunguza kodi ndio itakuwa kitovu cha mipango yake ya kuhuisha uchumi wa Marekani, iwapo atashinda katika uchaguzi wa Novemba.

Katika hotuba yake kubwa ya sera za uchumi aliyoitoa mjini Detroit, huku akikatishwa mara kwa mara na kelele za waandamanaji,Trump amesema kiwango cha kodi kwa wafanya kazi kitakuwa kidogo mno hivyo kuzalishwa kwa mamilioni ya kazi. Amesema anataka kufungua ukurasa mpya kwa uchumi wa Marekani.

Nae mgombea urais kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton akihutubia mkutano mjini Florida, amekosoa mikakati ya bwana Trump na kusema katu haitasaidia idadi kubwa ya wamarekani, lakini inasaidia watu ambao tayari wap juu. Hillary Clinton

Mipango yake ya kodi, itatoa afueni kwa mashirika makubwa na matajiri - kama yeye mwenyewe na watu waliomwandikia hotuba yake, au sio? Tunaenda kubadilisha uchumi, tunaenda kuwafanya matajiri kulipia sehemu yao ya kodi ili kuleta mabadiliko.Hillary Clinton , Mgombea Urais wa Marekani-Democratic

Wakati huo huo, msuguano mkali umeendelea baina ya Maafisa hao akiwemo mkurugenzi wa zamani wa CIA na mawaziri wawili wa mambo ya ndani, wametoa taarifa inayo mtuhumu Trump kwa kukosa uwezo, haiba na uzoefu wa kuhudumu kama rais wa Marekani. Wamebashiri kuwa huenda akawa Rais asiye na uwezo kwenye historia ya Marekani tangu taifa hilo kuanzishwa. Trump na Clinton kwa pamoja wanakosoa ushirikiano wa kibiashara wa Pacific

Katika kujibu mapigo Trump amesema watu hao ni miongoni mwa watawala wa Washington ambao wanapaswa kulaumiwa kwa kuifanya dunia kuwa sehemu hatari ya kuishi.

Trump anajitahidi kurudi kwenye ushindani baada ya wiki ambayo iliishia kumpa mpinzani wake wa chama cha Democratic, Hillary Clinton, uongozi wa wazi kwenye kura za maoni.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top