Trump aeleza mpango wa kupambana na ugaidi


Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump

Donald Trump ameeleza mpango wake wa kuifanya Marekani kuwa sehemu salama kwa kupambana na kile alichokiita kuwa ni ugaidi wa waislamu wenye itikadi kali. Amesema kama atachaguliwa kuwa rais wa marekani atabadilisha sera za mamabo ya nje za nchi hiyo zenye lengo la kujenga taifa kwa kuwa na sera zenye uhalisia.

Akihutubia mkutano wake katika jimbo la Ohio, mgombea urais kupitia chama cha Republican alisistiza juu ya umuhimu wa mpango wa muda wa kuzuia viza za waombaji wanaotoka katika nchi ambazo zina historia ya kueneza ugaidi ,na kupendekeza kuanzishwa kwa

mifumo ya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa akauti zao za mitandao ya kijamii. Aidha bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na nchi yoyote ile bila kujali tofauti za kiitikadi au mikakati akiwa na nia ya kusaidia kulitokomeza kundi la Islamic State
 Habari za Magazetiya Leo Jumanne August 16, 2016 bofya hapa

MANJI AJIUZULU YANGA bofya hapa

 Ajira zaidi bofya hapa


Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top