Spika wa Bunge Job Ndugai afunguka, aahidi kukaa na Ukawa

 
 Akijibu Maswali yamoja kwa moja ya Mwandishi wa habari, Spika wa Tanzania Job Ndugai, amesema anasikitishwa na Wabunge wa UKAWA na Tabia yao ya kutoka Nje. Japo ni haki yao kutoka nje lakini hivi karibuni imezidi. Japo itaendelea hivi tutakuwa hatujengi
nchi amesema.


Ameahidi yeye mwenyekiti wa Bunge na naibu Spika watakaa na UKAWA wamalize hili tatizo kwani haipendezi spika unakaa mtu anatoka nje.

Amesema Sasa Nchi hii Migogoro, utengano umezidi, ni jukumu letu kama Viongozi kumaliza hii hali.

Kasema Wabunge waliofungiwa ilitokana na matomeo ya sintofahamu. Kwani kabla ya kufungiwa tunaomba Mbunge afute kauli yake, arekebishe au alete ushahidi. Pale anapokaidi huitwa kutoa ushahidi lakini saa nyingine hukataa. Mfano kuna Mbunge alisema polisi wameleta Magari ya Washawasha 700. Tulipomwambia alete ushahidi akasema alisoma Kwenye JamiiForums. Kama bunge hatuwezi fanya kazi kwa kutengemea Mitandao

Anasema hii hali inayoendelea bungeni inachochea chuki na Migogoro. Ni bora sasa tukaa nchini kama taifa ili tumalize hii hali.

Anasema kama Spika hatavumilia vijembe na kejeli kuendelea Bungeni
Ni haki ya mbunge kutoka nje. Lakini wale waliobaki nao wanawashambulia waliotoka, hili nalo ni tatizo. Wabunge wakitoka nje mambo mengi huharibika. Inachafua hali ya hewa. Uchaguzi unapoisha, siasa huhamia Bungeni.

Tunachukulia Mbunge kama mtu mzima. Chama tawala na UKAWA na sisi tukae chini tuongelee hili swala.

Wabunge wamezoea kuona Spika na Naibu wake wakiwa wabunge wa kuchaguliwa, hii ya naibu Spika kuwa wa kuteuliwa wanahofu kwamba atakuwa anapokea maelekezo kutoka Sehemu Fulani. Naomba niwahakikishie kwamba, sisi hatupokei maelekezo kutoka sehemu yoyote bali tunatoa maamuzi yetu tunavyoona inafaa. Hivo watuamini. 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top