Paul Pogba
Paul Pogba amesema kuwa ni muda muafaka kurejea Old Trafford baada ya uhamisho wake wa Paundi 89 ulioweka rekodi ya dunia kwenda Manchester United.
Kiungo huyo mwenye miaka 23 anarejea tena klabuni hapo baada ya miaka minne alipoelekea Juventus kwa ada ya uhamisho wa pauni 1.5 milioni mwaka 2012.
Pogba, ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano ameongeza kuwa ''hii ni klabu sahihi kwangu kupata mafanikio ninayoyahitaji.''
Meneja wa Man U Jose Mourinho amesema Pogba atakuwa muhimili mkubwa wa klabu hiyo kwa kipindi kirefu kijacho.
United itailipa Juventus ambao ni mabingwa wa Italia Euro 105 milioni sambamba na Euro 5 milioni ikiwa hii ikitegemea kiwango chake kitakavyokuwa.
Uhamisho uliokuwa wa gharama na kushikilia rekodi ni wa Gareth Bale aliyetokea Spurs kwenda Real Madrid ukiwa ni Paundi 85.Pogba akiwa jijini Manchester
Pogba aliyeisaidia Ufaransa wenyeji wa michuano ya Euro 2016 kufika fainali ameshinda taji la Serie A katika miaka yote minne ndani ya klabu yake.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)