NEWS ALERT: ASKARI POLISI WANNE WAUWAWA USIKU HUU HUKO MBAGALA MMBANDEJIJINI DAR ES SALAAM


Taarifa iliyotufikia usiku huu inaeleza kuwa, kuna tukio la kuuwawa kwa Askari Polisi wanne na raia kadhaa kujeruhiwa lililotokea huko Mbagala Mmbande 




jijini Dar.
Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi na kuanza kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi wanadaiwa kuondoka na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.
ASKARI WALIOFARIKI ni
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU NA
G9544 PC TTITO.
Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea mnamo saa 1: 30 ni katika tukio la UVAMIZI WA BANK CRDB MBANDE na inadaiwa kuwa wahalifu hao waliondoka na silaha moja aina ya SMG.
Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva.
Inadaiwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki. 
Gari la Polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa kwa risasi.

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amethibitisha na kusema: "Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi hapa mbagala lakini kwa taarifa kamili ntazitoa kesho kwakuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi".
-------------------------------------------
"Usiku huu nimefika Mbande-Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.
Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.
Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu."

Mwigulu Nchemba
23.08.2016

Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa jumla ya askari wake wanne wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya majambazi kuvamia tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande, wilayani Temeke, Dar es Salaam.

Akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha Redio One Stereo leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema watu kadhaa wamekamatawa na msako unaendelea ili kuwapata waliotekeleza unyama huo.

Sirro amesema taarifa kutoka eneo la tukio zinaonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na baada ya kufanya mauaji hao, walivamia kituo cha polisi cha Mbande kisha wakavunja stoo na kuchukua sare ya askari na silaha.

Akielezea namna tukio hilo lilivyotokea, Kamanda Sirro amesema wahalifu hao walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana lindo katika taasisi hiyo ya fedha na kuibuka ghafla na kuanza kurusha risasi.

Kwa mujibu wa Sirro, gari la polisi limechakazwa kwa risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia na ndiye aliyeweza kutoa taarifa na maelezo ya namna tukio lilivyofanyika.

“Watu kadhaa wamekamatwa na tunaendelea na msako. Tunawataka wakiwa hai au wafu,” amesema Kamanda Sirro huku akiwataka watu kujihadhari na yeyote anayejitambulisha kwao kuwa ni askari bila kuonesha kitambulisho.

Ameendelea kusema kuwa baada ya operesheni ya kukomesha mtandao wa wahalifu kama hao na wengine kukimbilia nchi jirani, masalia wameanza kujikusanya na kutekeleza matukio ya mauaji huku askari wakilengwa.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba akimjulia hali Raia aliyejeruhiwa
Waziri Nchemba na Kamanda Sirro wakiwa eneo la tukio
Gari ya Polisi ikiwa imezagaa Risasi








Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top