Mrema amkumbusha Lowassa mwaka 1992


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema amesema Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa angefuata ushauri aliompa wa kuhama CCM mwaka 1992 wangeingia
Ikulu, 1995.

“Hata angekuja Lowassa sasa, nitamuuliza mwaka 1992 wakati natoka CCM nilikwambia tutoke sasa maji yamechemka tukiweka unga tutapata ugali, ukagoma Lowassa,” amesema Mrema jana alipozungumza na wanachama wa Chama cha Waendesha Bodaboda Wilaya ya Kinondoni (Chabbowiki).


Mrema amesema Lowassa aliamua kuendelea ‘kula kidogo’ na kuendelea kubaki CCM hadi alipotaka kugombea urais na jina lake kukatwa, akahamia upinzani.



Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top