Wanachama watatu wa klabu ya Yanga, Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim Abdallah ambao hawa ni wajumbe wa klabu hiyo waliochaguliwa na wanachama katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo wameenguliwa kwenye nyadhifa zao baada ya mwenyekiti wa klabu kudai viongozi hao wamekiuka maadili ya klabu
Amesema kwamba wajumbe hao kwa nyakati tofauti wamekua wamekua wakizozana na viongozi na kudiliki kuwaambia wachezaji wadai posho na kuzungumza na baadhi ya vyombo vya habari pasipo idhini yake
Hata hivyo Manji amewashangaa wanachama wa klabu hiyo kuhusiana na swala lao la kumchagua Hashim Abdalah kua mjumbe wa kamati ya utendaji wakati alihusika kufungwa na Simba bao 5-0 yeye akiwa mwamuzi wa mechi hiyo.
Aidha katika hatua nyingine Manji amewataka wanachama wa klabu hiyo kubadili mfumo wa katiba kwani katiba ya sasa haina uwezo wa kuleta maendeleo ndani ya klabu hiyo.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)