MANJI AJIUZULU YANGA



Habari zilizoenea kwenye mitao ya kijamii ni kwamba Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ameamua kujiuzulu wadhifa wa uenyekiti katika klabu hiyo pamoja na kusitisha zoezi la kutaka kuikodi timu
hiyo kwa miaka 10 kama ilivyokuwa dhamira yake hapo awali.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya Yanga, inadaiwa kuwa bosi huyo ameamua kukaa pembeni ikiwa ni baada ya kuibu kwa mijadala mikubwa na baadhid ya watu kupinga uamuzi wake wa kutaka kuikodi Yanga.

“Natukanwa sana na baadhi ya matajiri ambao ni wapenzi wa Yanga…hawapendi mimi niwepo pale. Pesa ni yangu natoa kwa mapenzi niliyonayo kwa klabu yangu…kwanini nitukanwe wakati sipati maslahi yoyote? Najiuzulu,” Ni kauli ya mwenyekiti wa Yanga SC ambaye ametangaza kujiuzulu kufuatia kusakamwa na hasa baada ya kuomba kuichukua Yanga kwa miaka 10. (kwa mujibu wa facebook page ya Naipenda Yanga).

Hata hivyo kumekuwa na vikao mbalimbali kumsihi Manji abadili maamuzi yake lakini inaonekana amechoka na ameamua kuibwaga Yanga.

Tayari Reginald Mengi ameonesha nia ya kuingia Yanga endapo Manji ataondoka.

Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu August 15, 2016 bofya hapa


 Ajira zaidi bofya hapa


Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top