KABLA YA KUANZA KWA VPL 2016/17, MANARA ATOA ONYO BODI YA LIGI


Zikiwa zimesalia takribani siku 14 ili kuanza kwa msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania msimu wa 2016/2017, afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema hatarajii kuona mapungufu yaliyojitokeza kwenye msimu uliopita yaani 2015/2016.

Manara alizungumza mara baada ya mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura kusema kwamba, msimu uliopita waamuzi walijitahidi kusimamia sheria 17 za soka kwasababu hadi ligi inamalizika hakuna mwamuzi aliyefungiwa kutokana na kuchezesha bila kufata sheria.

Kauli hiyo imepingwa na Manara ambaye amesema, klabu ya Simba ilipeleka malalamiko yasiyopungua nane juu ya maamuzi mabovu yaliyoihusha timu yao lakini hakuna lalamiko hata moja lililofanyiwa kazi wala kujibiwa.

“Bodi ya ligi wamesema msimu uliopita kulikuwa na ubora kwenye uamuzi, sisemi uongo lakini siyo kweli, msimu uliopita kulikuwa na uvundo kwenye maamuzi. Simba tumelalamika karibu mechi nane kwa kutuma malalamiko yetu kwa barua rasmi na hawakutoa maamuzi wala kusema lolote. Kama wao waliona ligi ya mwaka jana ilikuwa na maamuzi mazuri, itakuwa ni kituko,” amlisema Manara.

Wakati huohuo Manara akasema hatajii pia kuona mambo kadhaa yaliyojitokeza wakati wa msimu uliopita yakijirudia tena, timu kubadilisha kituo bila sababu za msingi wala timu kuruhusiwa kwenda kushiriki mashindano yasiyo rasmi na kusababisha ligi kusimama.

“Ligi iliyopita ilikuwa na changamoto nyingi mno, ilifika mahali timu inabadilisha kituo, ugenini inakuwa nyumbani na nyumbani inakuwa ugenini hatupendi kuona haya mambo yanajitokeza tena wala hatutarajii kuona vitu hivyo vinatokea,”.

“Jambo hili lilitokea kwenye mechi ya Yanga na Ndanda, halijawahi kutokea sehemu yeyote duniani tangu dunia imeumbwa hatutarajii hilo jambo litokee tena. “

“Msimu uliopita ligi ilisimama kupisha timu iliyokwenda kucheza bonanza, hatutarajii hayo yatokee tena kwasababu hata hao wadhamini wanaotoa hela watachoka kwamba kila siku ligi inamalalamiko. Hizi siyo changamoto ni matatizo kwa TFF na Bodi ya Ligi.”

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top