Tundu Lisu
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa na polisi muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa
Ikungi, Singida.
Ikungi, Singida.
Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwake kwenye mtandao akisema: “Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida.
--------- Ujumbe alioandika Tundu Lissu------
Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida.
Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki.
Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander Singida nikamatwe.
Apparently kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam. Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka.
It's likely nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi.
Kwa vyovyote itakavyokuwa, there's no turning back. There's no shutting up.
Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or in jail, as long as I've a voice to speak with.
Ujumbe toka CHADEMA:
Ni kweli. Tunaweza kuthibitisha kwa vyombo vya habari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama Mh. Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Singida kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.
Polisi wamemkamata jioni hii baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara alioufanya Ikungi jimboni kwake kwa kile walichosema kuwa ni maelekezo kutoka juu hivyo anapaswa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani Singida. Taarifa kutoka kwenye mfumo wa chama mkoani humo zimesema muda mfupi uliopita ndiyo amewasili kituoni hapo na kupelekwa Ofisi ya RCO Singida.
Tayari viongozi wa chama mkoani humo wako katika eneo hilo ili kuhakikisha Lissu anapata haki zake kama inavyostahili huku pia chama ngazi ya taifa, hususan Ofisi ya Katibu Mkuu, ikifuatilia kwa ukaribu kujua sababu hasa ya kushikiliwa kwake na kutoa msaada wa haraka kadri itakavyohitajika. Tutaendelea kuwajuza kuhusu suala hili.
Makene
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)