Agizo la Rais Magufuli Laanza kutekelezwa mgodi wa Geita

Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Geita la kuwagawia wananchi mabaki ya mawe maarufu kama Magwangala kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita GGM umeanza kutekelezwa
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo yupo katika ziara ya kikazi katika mgodi huo kwa kutafuta sehemu ambayo wachimbaji watayaweka na kuyachenjua kwa ajili ya kuyagawa kwa wananchi.


Akiongea mara baada ya ziara hiyo Mhe. Muhongo amesema kuwa agizo la Rais lilikuwa ni baada ya wiki tatu lakini kwa kuwajali wananchi wa eneo hilo wameamua kuanza zoezi hilo mapema kwa ajili ya utekelezaji wa agizo la rais.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Emanuel Kiunga, amesema kuwa serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wabunge wa mkoa huo na baadhi ya viongozi wametafuta maeneo ya kuweka Magwangala hayo kwa ajili ya kuyahifadhi.


Wakizungumzia maeneo hayo yaliyotengwa kwa ajili ya zoezi hilo baadhi ya wabunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa viti Maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Upendo Peneza, na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma wamesema serikali lazima iwe makini na mawe hayo pamoja na kuwajali wananchi wa maeneo yaliyotengwa.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top