Yanga yafungwa na Medeama michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika

 
Yanga imeshindwa kutamba mbele ya Medeama kwa mara nyingine tena kwenye michuano ya kimataifa baada ya kukubali kipigo cha bao
3-1 dhidi ya Medeama kwenye mchezo wa Kundi A wa michuano ya kombe la shirikisho Afrika uliochezwa huko Ghana. Matumaini ya timu ya Yanga kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika yameendelea kua finyu baada  kukubali kupokea kichapo hicho.
Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kushika mkia katika msimamo wa kundi A linaloongozwa na TP Mazembe wenye alama saba wakifuatiwa na Mo Bejaia na Medeama ambazo kila mmoja amefikisha alama tano.
.
Katika mechi ya leo bao la kufutia machozi kwa upande wa Yanga limefungwa na Saimon Msuva kwa mkwaju wa penati iliyosababishwa na Obrey Chirwa aliyechezewa mazambi ndani ya box

Mabao ya Medeama yamefungwa na Daniel Amoah na Abbas Mohamed ambae ametupia kambani mabao 2 mguu mwake.



Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top