Watu wasiopungua sita wauawa katika kituo cha biashara Munich Ujerumani


Askari polisi karibu na kituo chakibiashara cha Olympia, Munich.

Washambuliaji waliingia wakifyatua risasi katika kituo cha kibiashara cha Olympia karibu na uwanja wa Olimpiki mjini Munich (Bavaria) na kuwaua watu wasiopungua sita, polisi imeliambia shirika la habari la DPA.

Chanzo cha polisi kiliyonukuliwa na shirika la habari la AFP, kimesema mpaka sasa angalau watu 6 wameuawa katika shambulio hilo, linaloaminiwa kuendeshwa na watu watatu wenye silaha.

Polisi ya Ujerumani, ambayo pia inasema watu kadhaa wamejeruhiwa, inadhani kuwa washambuliaji watatu ndio wamehusika na shambulio hilo, na mpaka sasa haijulikani waliko. "Mashahidi wanasema wamewaona watu watatu wenye bunduki, " polisi ya Munich imebaini kwenye Facebook. Wakazi wa mji wa Munich wametakiwa kusalia nyumbani. Eneo la kibiashara limezingirwa serikali imeendelea na zoezi la kuokoa watu waliokuwa ndani ya kituo hicho cha kibiashara.

Gazeti la Münchener Abendzeitung limeandika kwamba shambulio hilo limesababisha vifo vya watu zaidi ya 15. Vituo vya televisheni vya Ujerumani vimekua vikionyesha magari kadhaa ya huduma za dharura karibu na kituo cha kibiashara. Kwa mujibu wa kituo cha NTV, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bavaria imethibitisha ripoti ya vifo vya watu watatu lakini chanzo cha polisi kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP kimesema watu 6 ndio wameuawa katika shambulio hilo.

Mfanyakazi mmoja ambaye yuko kituo hicho cha kibiashara ameliambia shirika la habari la REUTERS kwamba kumekuwa na milio mingi ya risasi, na wafanyakazi wa maduka walilazimika kufungiwa katika majengo hayo.

Kwa mujibu wa gazeti la BILD, mmoja wa washambuliaji aliwapiga risasi watu wengi kabla ya kukimbia akielekea kwenye kituo cha treni za mwendo wa kasi. hali bado ni tete katika mji wa Munich na viunga vyake. Baadhi ya barabara kuu zimefungwa na shughuli zimesimama.
 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top