Wabunge chadema kuhojiwa kwa kukiuka agizo la kutofanya mikutano



Jeshi la polisi mkoani Arusha, limewaita kwa mahojiano, mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo, mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso na Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu,Jubilate Mnyenye kutokana na kupuuza agizo la kutofanya
mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.


Mwingine ambaye ametakiwa kwenda kuripoti polisi ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta.


Wakizungumza jana baada ya kukabidhiwa barua za wito wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka kutakiwa kuripoti ofisi ofisi ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.


Parreso alisema,walipokea barua jana saa sita mchana na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane lakini wakampigia na kumweleza wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na akakubali.


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkombo alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top