Uturuki yatangaza hali ya hatari

 
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ametangaza hali ya hatari itakayodumu kwa miezi mitatu ili kutoa nafasi kwa mamlaka kuchukua hatua stahiki dhidi ya wanaoshukiwa kushiriki mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa juma lililopita.

Erdogan, ambaye alianzisha hatua ya kamata kamata katika taasisi mbalimbali tangu baada ya mapinduzi yaliyoshindwa, amesema hatua hiyo inazingatia katiba ya Uturuki na hajakiuka utawala wa sheria wala uhuru wa raia wa Uturuki.

Hali ya hatari, ambayo itaanza kutekelezwa mara tu baada ya kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali , itamruhusu Rais na Baraza kufanya kazi za bunge kupitisha sheria mpya na kuweka na kuweka mipaka au kusimamisha kwa muda baadhi ya haki na uhuru wa raia inapolazimika kufanya hivyo.

Erdogan alitoa tangazo hilo akiwa kwenye matangazo ya moja kwa moja kwa njia ya Televisheni mbele ya mawaziri wa Serikali baada ya mkutano wa baraza la usalama la Taifa.

Katika hatua nyingine, Majerali wa jeshi wameshtakiwa rasmi wakihusishwa na mapinduzi ya juma lililopita, pia imetangazwa kuwa majaji wa kijeshi na waendesha mashtaka wanafanyiwa uchunguzi.

Halikadhalika mamia ya shule na taasisi za kielimu zimefungwa.waalimu na wana taaluma ni sehemu ya maelfu ya wanajeshi, wafanya kazi wa umma na wengine wanaoshukiwa kuiangusha serikali, mpango unaodaiwa kuongozwa na Kiongozi wa Kidini aishie uhamishoni nchini Marekani, Fethullah Gulen. Wanafunzi hawa wanaeleza hatua hii ina maana gani kwa mustakabali wa maisha yao

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top