Simba inasherehekea wiki maalum iliyo Batizwa Jina la Simba Week ambayoImezinduliwa Leo na Rais wa Simba Sport Club Ndugu Evans Aveva na hufikia kilele chake Tarehe 8 Mwezi Agosti. Mwaka huu siku hii ya Simba week itakuwa na uzito wa kipekee kwani Klabu ya Simba itakuwa inaanza Sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya klabu Hiyo. Sherehe za Wiki ya Simba zinaenda sambamba na dhima yetu ya kuendeleza Mabadiliko chanya ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha mwaka mzima.
Katika Kipindi Hiki Simba Sport Club imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku maalum kwaajili ya kufurahi, kuwatambulisha Rasmi wachezaji,Jezi za timu na kujiandaa kwa Msimu Mpya, siku hii imekuwa Maarufu kama Simba Day. Tangu Ianzishwe imekua ikiboreka Siku hadi siku, mwaka huu Imeona ni Muhimu kuiboresha zaidi na hususani kuangalia Mchango wa timu Hiyo kwa Jamii inayoizunguka.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)