Mbunge wa jimbo la Mlimba Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga (CHADEMA)
Leo mahakama mkoani Morogoro yatoa uamzi wa kesi mbili leo za wabunge wa Chadema hivi ndivyo maamzi ya Mahakama
1. Mh. PETER AMBROS LIJUALIKALI ametangazwa kuwa Mbunge halali wa Ifakara mjini.
SABABU ZA USHINDI;
Mashahidi Kujichanganya.
Kutopeleka Malalamiko Kamati ya Maadili.2. Mbunge wa jimbo la Mlimba kupitia CHADEMA Suzan Kiwanga, ameshinda kesi ya uchaguzi katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Morogoro.
Katika Uchaguzi mkuu wa 2015 Jimbo la Mlimba, Suzan Kiwanga alishinda kwa kupata kura 40,068 dhidi ya Mpinzani wake wa karibu Godwin Kunambi wa CCM aliyepata kura 34,883.
Jimbo la Kilombero Peter Lijualikali wa CHADEMA alishinda kiti cha ubunge kwa kupata kura 62,158 wakati mpinzani wake wa karibu, Abubakar Assenga wa CCM alipata kura 44,092.
Katika hukumu kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Kilombero na Mlimba ambayo imesomwa leo.
Kutokana na majimbo hayo kuwa na historia ya Vurugu zinazotokana na matukio ya kisisasa, jeshi la Polisi lilimarisha ulinzi mkali katika viwanja vya ukumbi wa Halmashauri ya Kilombero ikosizwa kesi ya mbunge wa jimbo hilo na katika mahakama ya wilaya, inakosikilizwa kesi ya mbunge wa jimbo la Mlimba.
Kesi ya Kilombero na Mlimba zimesilizwa LEO
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)