News alert:Rais Magufuli alitolea ufafanuzi suala la Elimu za Wakurugenzi wapya

Rais Dkt Magufuli leo amelazimika  kulitolea ufafanuzi swala la elimu za Wakurugenzi kutokana na minong'ono mingi iliyoibuka na kuibua mijadala juu ya watu mbalimbali kuhoji elimu za Wakurugenzi hao wapya, ameongea hayo muda mfupi katika hafla ya kiapo cha maadili kwa Wakurugezi na Wakuu wa wilaya watatu ambao awali ama hawakuwepo
au wameteuliwa upya, 

Rais    Dkt Magufuli amesema kuwa asilimia kuwa ya Wakurugenzi wana elimu ya Shahada ya pili (Masters) na wengine waliobaki wana elimu ya shahada ya kwanza hakuna hata mmoja aliye na elimu chini ya hapo "Kati ya nafasi ambazo nilikuwa makini sana ni hii ya Wakurugenzi maana nyinyi ndio watendaji wakuu wa kusimamia Ilani ya CCM " alisema Dkt Magufuli
Akizungumzia Swala la Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya Same Anaclaire Shija, Rais Magufuli alisema "Huyu Shija wanayesema kuwa ana Diploma na ni mfanyakazi wa hoteli sio kweli, huyu dada mnayemwona hapa ana Shahada ya Pili (Masters) kwahiyo wanaomzushia uongo nawaombeni waandishi wa Habari mpigeni picha ili mkawaonyeshe hao wanaosema kuwa ana Diploma..washindwe na Walegee" alisema Rais Dkt Magufuli

Katika hatua nyingine Rais Dkt Magufulia aliongelea suala la ambalo lipo kwenye mitandao ya kijamii kumuandika Luhende kama Msomi mwenye cheti cha hotel Management wakati ana Masters na alikuwa mkaguzi wa elimu wa kanda.

Rais anasema amepitia kwenye mtandao mmoja wa kijamii akaona comment za watu juu ya Luhende akabaki kucheka tu,amemsimamisha Luhende na kuwataka waandishi wa habari wampige picha na waende Sinza kumpiga picha Luhende Meneja wa Hotel nakuzisambaza mitanadaoni

Rais pia anasema anawafahamu Wakurugenzi wake wote,anasikia malalamiko kwenye mitandao ya kijamii,amewaambia wajishangilie wao na si kusikitika kwa kutokushangiliwa na mitandao ya kijamii,anasema hao wasioshangilia kwenye mitandao ni maadui zake,..."Watachonga sana lakini wataka kimya"

Rais anasema zamani nafasi za ukurugenzi zilikuwa "deal",na pale TAMISEMI kulikuwa na mtandao wa kuhongwa ili kuwapatia watu ukurugenzi,aliishagiza Waziri awaondoe wapo watatu pale utumishi ambao kazi yao ilikuwa kuhongwa na kugawa vyeo vya Ukurugenzi.

Rais anasema Wakurugenzi wote aliwapitia jina kwa jina na ndio maana hasafiri ili kufanya mambo yeye mwenyewe na wakati mwingine hulala hata saa nane ili kujiridhisha mambo.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top