Polisi wa Dallas watano waliuawa wakati wa kupinga mauaji ya risasi dhidi ya wamarekani weusi yanayofanywa na polisi
Mtu aliekua na silaha wakati wa mzozo na polisi wa Dallas amesema kuwa alikasirishwa na kitendo cha polisi kuwapiga risasi watu weusi na
alitaka kuwauwa polisi wazungu , ameseama mkuu wa polisi wa mji huo.
Mshukiwa huyo ameiambia polisi kwamba alifanya hivyo bila ushawishi wowote , Mkuu wa polisi David Brown aliwaambia maripota.
Maafisa watano wa polisi wa Dallas waliuawa na wengine saba kujeruhiwa na wakati wa maandamano dhidi ya visa vya polisi kuwapiga risasi wamarekani weusi, zimeeleza mamlaka.
Watu watatu wamewekwa mahabusu. Mkuu wa polisi wa Dallas amesema mshukiwa aliuliwa na vilipuzi vilivyotegwa na polisi kwenye jengo alimokuwemo
Bwana Brown amesema kuwa mshukiwa alialiuawa wakati polisi walipotumia vilipuzi vilivyotegwa kwa roboti kumaliza wasi wasi wa ghasia katika jengo ambamo alikua amezuiliwa.
Maandamano hayo yamejiri baada ya mauaji ya wiki hii ya wamarekani weusi Philando Castile wa jimbo la Minnesota na Alton Sterling wa Louisiana.
(Breaking news:Polisi watano wauawa Dallas Marekani bofya hapa)
Rais arack Obama, ambae anahudhuria mkutano wa Nato nchini Poland, ametaja mashambulio hayo kama "mfulurizo wa ghasia zilizpopangwa na mashambulio yasiyokubalika dhidi ya watekelezaji wa sheria".
Amesema kuwamji wote wa Dallasuna majonzi na "hali hii inaigusa jamii yote ya polisi wa Marekani imesikitika kwa kuwakosa wenzao".
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)