Na Ally Mwandike
Baada ya kamati ya maadili ya TFF kuweza kumfungia Jerry Muro kutojihusisha na soka kwa muda wa mwaka mmoja na kulipa faini ya milioni tatu,jambo hilo limezungumzwa na afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Sundey Manara kwa kusema
mkuu huyo wa idara ya habari na mawasilino wa mahasimu wao katika soka la bongo aliponzwa na kuzungumza na kuvuka mipaka ya kazi yake.
Manara amegusia suala hilo alipokutana na Jerry Muro alipomtembelea nyumbani kwake hivi karibuni sambamba na baadhi ya mashabiki na wanachama wa young Africans kwa lengo la kumkabhi fedha za mchango kiasi cha Shilingi milioni moja na elfu hamsini na tano (1,055,000) kama mchango wao ambazo utasaidia kwenye matibabu yake atakapokwenda nchini India mwishoni mwa juma hili.
Mbali na kuzungumza udhaifu wa Muro ambao umemsababishia kufungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja, Marara pia alitoa shukurani kwa msaada wa fedha walioupokea kutoka kwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa Young Africans
Hata hivyo Manara amesema kwamba mapambano yake kwa Yanga atakaporejea kutoka nchini India baada ya matibabu yatakua pale pale kwani amedai kua maishani mwake hawezi kufurahia mafanikio ya Yanga
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)