Wasichana wamejikuta wakipata madhara ya ndoa za utotoni na kuhatarisha maisha yao
Mahakama kuu nchini Tanzania jana ilidhinisha umri halisi wa kuolewa kwa mtoto wa kike kuwa miaka
18. Wasichana wenye umri wa miaka 14 huolewa kwa ridhaa ya wazazi wao.
Mahakama kuu imetoa muda wa mwaka mmoja kuhakikisha kuwa Serikali inasahihisha sheria ya mwaka 1971 kifungu cha 13 kinachoruhusu Mtoto wa kike kuozwa akiwa na umri miaka 14
Wasichana wanaoolewa katika umri huu mara nyingi wanakabiliwa na unyanyasaji wa majumbani sambamba na kutengwa na jamii huku wakipewa nafasi ndogo kwa ajili ya elimu na ajira.
Huu ni ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa Tanzania katika kupigania haki za watoto na sasa itakuwa rahisi kuwaokoa wasichana wanaoathirika na utamaduni wa kuozeshwa wakiwa wadogo.
Uamuzi huu umekuja wakati Bunge kupitisha sheria ya kifungo cha miaka 30 ama faini ya dola 2500 kwa mwanaume atayebainika kumuoa ama kumpa mimba mwanafunzi.Hata hivyo sheria hii inawatenga maelfu ya wasichana ambao si wanafunzi.
NAFASI TANO ZA KAZI BOFYA HAPA
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)