Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa
Selestine ameziasa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutimiza masharti ya kupata vibali vya
kuishi na kufanya kazi Tanzania kwa wachezaji na wataalamu wa kigeni
wakiwamo makocha na madaktari kabla ya kuingia nao kandarasi za ajira.
Masharti hayo ni vibali vya kufanya kazi nchini, visa za kuishi nchini,
vibali vya kucheza mpira wa miguu nchini, vibali vya kufundisha mpira na
vibali vya watalaamu wengine kama madaktari na hayo ni kwa mujibu wa
Idara ya Uhamiaji na mamlaka nyingine za serikali na kanuni za
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini ,TFF.
“Mchezaji au mtaalamu ye yote anapokuja nchini na kuanza mazoezi na timu
yo yote anachukuliwa yuko kazini. Tusingependa watu wapate usumbufu.
Kama Katibu Mkuu na mtendaji mkuu, nimepata maelekezo kutoka mamlaka
zinazohusika kuwa nifuatiulie kuwa TFF kamamratibu mkuu wa mchezo wa
mpira wa miguu ina jukumu la kuhakikisha wanachama wake wanafuata
taratibu.natakiwa kufuatilia,” amesema Selestine.
“Vilabu vihakikishe vyeti vya taaluma vinawasilishwa TFF kwa ajili ya
ukaguzi kabla ya kutiliana kandarasi na wachezaji au walimu. . Ni vema
wakafanya uratatibu wa kuhakiki Hii itaviepusha vilabu na gharama za
fidia au kesi za madai endapo mamlaka za serikali au za mpira zitasita
kumruhusu mhusika kufanya kazi nchini,” amesema.
Vilevile Katibu Mkuu wa TFF amezitaka klabu kumalizana na wachezaji na
wataalamu zinaoachana nao kabla ya kufikiria kuingiza wapya.TFF tayari
ina barua kadhaa za madai ya wachezaji na watumishi wa vilabu
waliomaliza au kukatishwa mikataba yao bila kulipwa mafao yao.TFF
inawataka kumaliza masuala haya ili kuweza kujikita vema katika kupanga
safu zao kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi.
Wakati huohuo, huo huo TFF imeagiza klabu kuendelea na usajili kabla ya
Agosti 6, 2016 ambayo itakuwa siku ya mwisho na kwamba hakutakuwa na
muda wa kuongezwa kwa klabu ambayo itashindwa kukamilisha usajili kwa
wakati.
Haya hapa majina 1,091 ya wadaiwa yaliyotangazwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)